Biashara ndogo ndogo zinazolipa Tanzania

Biashara ndogondogo zinajumuisha biashara zote zenye mitaji chini ya shilingi milioni tano fedha za kitanzania. Mara nyingi zimeajiri watu chini ya watano. Biashara hizi huendeshwa na wajasiriamali wadogo wadogo pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati.

Kutokana na wimbi la upungufu wa ajira rasmi sasa upo uhitaji wa hali ya juu kuweza kupata kazi kwa ajili ya nguvu-kazi iliyopo mtaani. Kuupata mtaji ni sehemu ya kutatua changamoto hii lakini baada ya hapo mtaji huo unapaswa kufanyiwa kazi katika shughuli inayolipa na yenye manufaa kwa mtu binafsi, jamii na Taifa kwa ujumla.

Kila mmoja anapaswa kufanya utafiti binafsi ili kutambua ikiwa wazo la biashara litafaa katika eneo husika. Ili kukusaidia kufanya maamuzi jitahidi biashara hiyo itemize mambo haya;

Uhitaji (Need): Ni lazima biashara iwe inahitajika na inawafaa wateja wa jamii husika. Biashara tunaanzisha kwa ajili ya kuhudumia jamii ili ikubali kukupatia hela. Kuwa makini unapoanzisha biashara kwa hobbie ama hamu yako binafsi. Ni lazima ihitajike na wateja. Zingatia.
Ugumu wa kuianza (Entry): Biashara zinazoweza kufanywa na yeyote wakati wowote huwa na ushindani mkubwa sana. Lakini hilo lisikutishe, unaweza kuichukua biashara ya kawaida na ukaiweka katika mtindo ambao kuna ugumu wa kuiba wazo lako kirahisi. Maeneo mazuri kuweka nguvu ya ushindani wako ni 1. Ujuzi wa hali ya juu, 2. huduma kwa wateja na 3. mazingira. Epuka kushindana kwa kutumia bei pekee maana inaumiza wafanyabiashara wote mnaohusika.
Unayoiendesha (Control): Kimsingi kuendesha mambo yako mwenyewe ni moja ya vitu ambavyo humvutia mjasiriamali kufungua biashara yake mwenyewe. Jitahidi biashara unayoichagua iwe ni ambayo unao uwezo wa kuitawala kwa kiasi kikubwa. Unaweza kuanza biasha hata kama hujaitawala vizuri lakini jitahidi baada ya hapo kuzingatia kuutafuta ujuzi ili uweze kuitawala. Unaweza kutumia makocha wa kibiashara kuharakisha jambo hili.
Inayoweza kupanuka (Scalable): Baadhi ya biashara hupatwa na tatizo la kuharibiwa kutokana na ukuaji wake yenyewe. Mfano kibada cha chipsi kinapozidiwa na wateja kiasi cha kupata sifa mbaya ya kwamba kina foleni sana na mwishowe huduma kuwa mbovu na biashara inakufa. Inajiua yenyewe, ajabu hii! Kitu muhimu ni kubakia macho kila siku kutazama namna unaweza kuiboresha kwa uendelevu biashara yako (KAIZEN). Mfano kuongeza majiko, kuongeza wafanyakazi na kuhama au kupanua eneo la biashara Zaidi kwa kuongeza eneo la kupaki usafiri.
Muda (Time): Pale unapoanzisha biashara weka akilini moja kwa moja suala la muda. Biashara iwe katika hali ambayo kutokuwepo kwako hakuathiri sana uendeshaji wake. Hii itasaidia kuwa hata unapopata dharula za hapa na pale biashara iweze kuendelea. Suala la muda linaweza kuachwa mwanzoni unapoanzisha biashara lakini kadri muda unavyoenda jitahidi kuiweka mifumo katika namna ambayo kazi itaendelea. Njia kama kuajiri wafanyakazi zaidi na wa kuaminika, kufunga kamera za usalama maana sio gharama sana siku hizi zipo hadi taa zenye kamera unayoiunganisha na simu!
Ukishalipata wazo lako la biashara unakaribishwa kujisajili na Mtandao wa Wajasiriamali wa Sahili kwa ajili ya kujitangaza na kujifunza zaidi kuhusiana na bidhaa na huduma za wajasiriamali Tanzania:

Zifuatazo ni baadhi ya biashara ndogondogo zenye uwezo wa kukupatia kipato kwa mtaji mdogo;

Uoshaji wa bodaboda na magari
Kuendesha bodaboda kwa mkataba
Kibanda cha chipsi
Kituo cha ufuaji wa nguo (Dry cleaner)
Duka la vitu vya nyumbani
Uzalishaji/utengenezaji wa sabuni
Uzalishaji/utengenezaji wa mageti na aluminiamu
Kuuza vitafunwa kama crips, vitumbua, maandazi na mihogo
Kutoa nakala na steshenari
Upigaji paspoti
Duka la dawa muhimu (DLDM)
Zote hizi na zinazoendelea ni biashara ambazo zinaweza kuanzishwa na wajasiriamali wadogo Tanzania:

  1.     Salon ya kike (Salon for ladies)
    
  2.     Salon ya kiume (Barber shop)
    
  3.     Biashara ya juisi za matunda (Fresh juice business)
    
  4.     Uuzaji wa mboga mboga (Selling vegetables)
    
  5.     Ushonaji wa nguo (Tailoring business)
    
  6.     Uuzaji wa urembo na vipodozi (Cosmetics and beauty products)
    
  7.     Uuzaji wa viatu (Selling shoes)
    
  8.     Uuzaji wa nguo za mitumba (Second-hand clothes business)
    
  9.     Biashara ya duka la dawa baridi (Selling over-the-counter medicine)
    
  10.     Kukodisha mitambo ya ujenzi kama vile “vibrators” na mashine za maji (Renting construction machines)
    
  11.     Shule ya chekechea (Daycare/Preschool)
    
  12.     Uchomeleaji wa milango na madirisha ya chuma (Metal welding business)
    
  13.     Biashara ya kuchakata taka (Waste recycling business)
    
  14.     Kuanzisha kituo cha mazoezi (Gym or fitness center)
    
  15.     Biashara ya kuuza maji ya kunywa (Bottled water selling)
    
  16.     Biashara ya kuboresha samani (Furniture refurbishing)
    
  17.     Uuzaji wa chakula cha mifugo (Animal feed selling)
    
  18.     Uuzaji wa mayai (Egg selling)
    
  19.     Shamba la kuku (Poultry farming)
    
  20.     Shamba la mbuzi (Goat farming)
    
  21.     Uanzishaji wa biashara ya duka la vipuri vya magari (Spare parts business)
    
  22.     Ukarabati wa vifaa vya umeme na simu (Repair of electronics and phones)
    
  23.     Studio ya picha na video (Photography and video studio)
    
  24.     Biashara ya kuuza na kusambaza mkaa (Selling and distributing charcoal)
    
  25.     Uuzaji wa gesi za kupikia (Selling cooking gas)
    
  26.     Uendeshaji wa kibanda cha matunda (Selling fruits)
    
  27.     Uuzaji wa mchele, unga, na nafaka nyingine (Selling rice, flour, and grains)
    
  28.     Biashara ya maduka ya rejareja (Retail shop)
    
  29.     Biashara ya maduka ya jumla (Wholesale business)
    
  30.     Kupaka rangi nyumba (House painting services)
    
  31.     Uuzaji wa vifaa vya ujenzi kama nondo, sementi na bati (Selling construction materials)
    
  32.     Utoaji wa huduma za kufua magari (Car washing services)
    
  33.     Biashara ya uuzaji wa vyakula kwa njia ya mtandao (Online food delivery business)
    
  34.     Uuzaji wa vifaa vya shule (Selling school supplies)
    
  35.     Kutengeneza na kuuza batiki na vitenge (Making and selling batik and kitenge fabric)
    
  36.     Uuzaji wa maua na mapambo ya ndani (Selling flowers and home decorations)
    
  37.     Biashara ya chakula cha mifugo kama mbwa, paka na ndege (Selling pet food)
    
  38.     Kukuza na kuuza samaki (Fish farming)
    
  39.     Biashara ya kuuza simu za mkononi na vifaa vyake (Selling mobile phones and accessories)
    
  40.     Kuanzisha duka la mbolea na pembejeo za kilimo (Selling fertilizers and agricultural inputs)
    
  41.     Kutoa huduma za kuweka nywele (Hair braiding and styling services)
    
  42.     Biashara ya ushonaji wa mashuka na vitambaa vya ndani (Making and selling bed linens and home fabrics)
    
  43.     Kuanzisha kioski cha kahawa na chai (Coffee and tea kiosk)
    
  44.     Biashara ya kuuza asali (Selling honey)
    
  45.     Biashara ya ufugaji wa nyuki (Beekeeping business)
    
  46.     Biashara ya kuuza vifaa vya michezo (Selling sports equipment)
    
  47.     Uuzaji wa bidhaa za plastiki kama ndoo, beseni na mikoba (Selling plastic goods)
    
  48.     Biashara ya urembo wa kucha (Nail beauty salon)
    
  49.     Uuzaji wa matofali na vifaa vya ujenzi wa nyumba (Selling bricks and building materials)
    
  50.     Biashara ya kuuza mbolea za asili (Selling organic fertilizers)
    
  51.     Uuzaji wa vifaa vya umeme kama taa na swichi (Selling electrical supplies)
    
  52.     Biashara ya kupaka rangi magari (Car painting services)
    
  53.     Uanzishaji wa biashara ya mtandao wa wifi kwa jamii (Community wifi business)
    
  54.     Kuanzisha kituo cha huduma za mtandao (Internet cafe)
    
  55.     Biashara ya kuendesha mabasi madogo (Operating a minibus service)
    
  56.     Kuanzisha duka la kuuza magari yaliyochakaa (Selling used cars)
    
  57.     Uuzaji wa bidhaa za mafuta kama petroli na dizeli (Selling petroleum products)
    
  58.     Kuanzisha kituo cha baiskeli za kukodisha (Bicycle rental service)
    
  59.     Biashara ya kusafirisha mizigo midogo (Small-scale logistics)
    
  60.     Uanzishaji wa kituo cha kubadilisha fedha (Currency exchange bureau)
    
  61.     Kuanzisha huduma za usafi wa nyumba (Housekeeping services)
    
  62.     Uuzaji wa vyakula vya kilimo kama vile viazi, mihogo na maharage (Selling agricultural produce)
    
  63.     Kuanzisha huduma za kupaka na kuchora kucha (Nail painting and art services)
    
  64.     Kuanzisha kituo cha kufua na kupiga pasi nguo (Laundry and ironing services)
    
  65.     Biashara ya kukodisha baiskeli za watoto (Kids’ bicycle rental service)
    
  66.     Kuanzisha banda la kuuza vinywaji baridi na maji (Cold beverages kiosk)
    
  67.     Kuanzisha biashara ya kuuza nazi na bidhaa zake (Coconut and its products business)
    
  68.     Biashara ya kuuza na kutengeneza mabegi (Bag making and selling)
    
  69.     Biashara ya kuuza vitabu na magazeti (Selling books and newspapers)
    
  70.     Uanzishaji wa biashara ya usafiri wa teksi (Taxi service)
    
  71.     Biashara ya kuuza bima (Selling insurance)
    
  72.     Kuanzisha huduma za uhamasishaji wa mitandao ya kijamii (Social media marketing services)
    
  73.     Kuanzisha banda la kutengeneza na kuuza sharubati (Juice bar)
    
  74.     Biashara ya kutoa huduma za ushauri nasaha kwa vijana (Youth counseling services)
    
  75.     Kuanzisha huduma ya kutoa huduma za kimtandao kama graphic design (Online services such as graphic design)
    
  76.     Biashara ya uuzaji wa samani zilizotumika (Selling second-hand furniture)
    
  77.     Biashara ya kuuza mavazi ya watoto (Selling children’s clothing)
    
  78.     Biashara ya kuuza vyombo vya jikoni (Selling kitchenware)
    
  79.     Kuanzisha kituo cha kusaga na kuuza unga wa mahindi (Maize milling and selling)
    
  80.     Biashara ya kuuza vyakula vya barabarani kama maandazi na samaki (Selling street foods such as donuts and fish)
    
  81.     Kuanzisha biashara ya usafirishaji wa mizigo kwa pikipiki (Motorcycle cargo transport)
    
  82.     Biashara ya kutengeneza na kuuza vipuli vya magari (Making and selling car accessories)
    
  83.     Kuanzisha biashara ya huduma za usalama kama walinzi (Providing security services)
    
  84.     Uuzaji wa vifaa vya kilimo kama mashine za kuvunia na kupandia (Selling farming equipment)
    
  85.     Biashara ya kuuza maua ya plastiki (Selling artificial flowers)
    
  86.     Biashara ya utalii wa ndani (Domestic tourism services)
    
  87.     Kuanzisha huduma za upimaji afya (Health screening services)
    
  88.     Biashara ya kupamba kumbi za harusi na sherehe (Event decoration services)
    
  89.     Kuanzisha biashara ya usambazaji wa maziwa (Milk distribution business)
    
  90.   Biashara ya kuuza mayai ya kuku wa kienyeji (Selling local chicken eggs)
    

Baada ya hapo yafaa kulifafanua wazo lako kiundani zaidi ili ulitawale kwa kuandaa mpango kazi wa biashara yako (Business plan). Ili kujua namna ya kuandaa soma blogu hii: Jinsi ya Kuandika Mpango wa Biashara (Business Plan) – Sahili

1 Like